New events
TAREHE YA KUFUNGULIWA CHUO DODOMA KAMPASI
Mkuu wa chuo cha elimu ya biashara cbe anawatangazia wanafunzi wote kuwa chuo kitafunguliwa tarehe 01/06/2020 katika kampasi zake zote.
Wanafunzi wa bweni wanashauriwa kuripoti kabla ya tarehe 01/06/2020
Wanafunzi wote wanapaswa kuzingatia yafuatayo:
1. Wanafunzi wa bweni wataendelea kukaa kwenye vyumba walivyopangiwa kabla ya chuo kufungwa.
2. Wanafunzi wa ngazi ya cheti na diploma1 “march intake” ambao hawajakamilisha usajili, wanaelekezwa kukamilisha usajili wao kuanzia tarehe 29 mei, 2020 hadi 05 juni, 2020.
3. Wanafunzi wanatakiwa kupakua ratiba ya masomo kwenye “saris account “ yao.
4. Wanafunzi wanashauriwa kuzingatia yafuatayo:
i. Kunawa mikono kwa sabuni kila mara katika sehemu zilizotengwa chuoni
ii. Kuepuka misongamano
iii. Kuvaa barakoa (masks) pamoja na kutumia vitakasa mikono (hand sanitizer) watakapokuwa chuoni au popote pale penye mkusanyiko wa watu.
5. Kuzingatia maelekezo mbalimbali yanayotolewa na wizara ya afya.
Maelekezo zaidi kuhusu mambo muhimu ya kuzingatia pindi wanafunzi watakapokuwa chuoni yanapatikana kwenye mbao za matangazo pamoja na tovuti ya chuo
CALL FOR PAPERS - (BEDC 2020)
We invite academicians,researchers,policy makers and other stakeholders to submit their research abstracts,papers,case studies and posters the 1st Business and Economic Development Conference(BEDC 2020).CLICK HERE TO READ MORE ABOUT THE CONFERENCE: