Watumishi wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Kampasi ya Dodoma, wakiongozwa na Mkurugenzi wa Kampasi Dkt. Kembo Bwana, walifanya ziara ya utalii Zanzibar. Katika safari hii, walitembelea vivutio vya kitalii kama Safari Blue, Msitu wa Jozani, na utalii wa kuangalia pomboo (dolphin) Kizimkazi. Ziara hiyo ilianza kwa kutumia treni ya mwendo kasi (SGR), ambayo imeleta mapinduzi makubwa ya kiuchumi na kibiashara nchini. SGR inarahisisha usafirishaji wa bidhaa na abiria kwa ufanisi zaidi, ikipunguza gharama za usafirishaji na kuchochea ukuaji wa biashara, hasa kwa sekta ya utalii.